Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) inashiriki Maonesho ya Nane Nane kitaifa
yanayofanyika katika Viwanja vya Maonesho vya Nzuguni jijini Dodoma.
TARURA inashiriki
maonesho hayo kwa lengo la kutoa elimu kuhusu kazi na majukumu yake pamoja na
kupokea maoni na malalamiko kutoka kwa wananchi.
Mkuu wa Kitengo cha
Uhusiano na Mawasiliano wa TARURA Bi. Catherine Sungura amesema kuwa TARURA
imejipanga kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo mbalimbali wanayoyasimamia
yanayohusu ujenzi wa miundombinu ya barabara nchini.
Kwa mujibu wa Bi. Sungura
baadhi ya maeneo hayo ni pamoja usimamizi wa matengenezo ya kawaida,
matengenezo ya maeneo korofi shughuli za maabara,mazingira na jamii.
"Kupitia wataalamu
wetu ambao wapo katika banda letu
tumejipanga pia kutoa elimu kwa wananchi na wadau wetu wengine namna
wanavyoweza kushirikiana na TARURA kuwezesha matengenezo madogo madogo ya
barabara kupitia vikundi vya kijamii," amefafanua Bi. Sungura
Aidha, ametoa wito kwa
wananchi kutembelea Banda la TARURA na
mabanda mengine ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI ambayo yanapatikana katika hema
linalosomeka "Government Zone Pavilion 2" ili wapate elimu na ufahamu
kuhusu taasisi hizo.
0 Maoni