Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa
Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Serikali
itaendelea kuziunga mkono na kushirikiana na taasisi zote za dini ili
kuleta na kuchagiza maendeleo na Ustawi wa wananchi.
Dkt. Biteko amesema hayo leo Agosti 17,
2025 wakati akimwakilisha Makamu Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuwa mgeni maalum
katika maadhimisho ya miaka 125 ya
Ukristo na Uinjilishaji katika Parokia ya Kome, Jimbo Katoliki la Geita.
“ Niseme Serikali itaendelea
kushirikiana na taasisi zote za dini katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo
na hii ni kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo” amesema Dkt. Biteko na
kuongeza kuwa Serikali inafarijika kuyokana na mchango wa taasisi za dini
kuwaletea wananchi maendeleo katika maeneo yao.
Sambamba na ibada hiyo ya Jubilei,
Dkt. Biteko ameongoza Changizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji kwa ajili
ya huduma katika makazi ya Masisita, Parokia ya Kome.
Akizungumza mara baada ya misa, Askofu
wa Jimbo Katoliki la Geita, Mhasham FLavian Kassala Maombi ya Baraka kwa
mchakato wa kupata viongozi na mchakato wa kupata viongozi sahihi katika
uchaguzi Mkuu ujao mwezi Oktoba, 2025.
Mhasham Askofu Kassala ametoa shukrani
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na
Serikali ya awamu ya sita kufuatia ushirikiano wa Serikali kwa taasisi za dini
ambazo zimekuwa chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali nchini.
Amesema huduma ya maji safi na salama
katika Kisiwa cha Kome bado ni changamoto hivyo, ameiomba Serikali kufanikisha
mpango wa upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa Kome.
“ Pamoja na kwamba hapa ni kisiwa na
tumezungukwa na maji, huduma ya maji safi bado ni ndogo na wananchi wenye uwezo
wa kupata maji ni wachache,” amesema Askofu Kassala.
Amesema Kanisa liko katika jitihada za
kusogeza huduma za jamii kwa kuongeza watawa zaidi ambo watatoa huduma za jamii
na hiyo wanahitaji huduma za haraka.
Dkt. Biteko amesema serikali itafanya
upembuzi ili kuhakikisha huduma hiyo ya maji ili kuhakikisha watawa wanapata
maji.
Amewaomba wakazi wa Kome kuzidisha
moyo wa ushirikiano sambamba na kuboresha mazingira na kupanda miti ili kulinda
na kurejeaha uoto wa asili.
Aidha, amechangia kiasi cha shilingi
milioni 10 huku akiwasilisha mchango wa shilingili milioni 50 kutoka kwa Rais
Samia Suluhu Hassan ikiwa ni sehemu ya kufanikisha azma ya kufanikisha
upatikanaji wa huduma ya maji katika makazi ya watawa Kome.
Awali akihubiri katika ibada ya
maadhimisho ya miaka 125 tangu kuanzishwa kwa utume katika Parokia ya Kome,
Askofu Mkuu wa Jumbo Kuu la Mbeya, Mhasham Gervas Nyaisonga amewataka waumini
kushikamana, kuvumoliana na kujenga maelewano katika jamii.
“ Tunapoadhimisha miaka 125 ya utume
tunitahidi kuelewq kuwa tunatakiwa kustawisha umoja na utulivu miongoni mwetu,
sisi ni wadhaifu tuna mapungufu tumgeukie Mungu na kuomba nguvu.” anesema
Askofu Mkuu Nyaisonga.
Akizungumzia uchaguzi Mkuu ujao,
Nyaisonga amewataka wakatoliki kufanya maombi maalum kwa saa 24 kuanzia Agosti
23-24 mwaka huu ili kufanikisha uchaguzi wa amani utakaowezesha upatikanaji wa
viongozi bora.
Na. Ofisi ya Naibu Waziri Mkuu na
Waziri wa Nishati
0 Maoni