Rais Samia kuongoza kuaga mwili wa Spika Mstaafu Ndugai

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisaini Kitabu cha Maombolezo mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma kwa ajili ya kuongoza waombolezaji kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai tarehe 10 Agosti, 2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiposhiriki ibada ya kuaga Mwili wa aliekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Hayati. Job Ndugai katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo August 10,2025.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson wakishiriki ibada ya kuaga Mwili wa aliekuwa Spika wa Bunge la Tanzania Hayati. Job Ndugai katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo August 10,2025.

Viongozi mbalimbali akiwamo Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wakishiriki ibada kabla ya kuaga mwili wa Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Job Yustino Ndugai katika viwanja vya Bunge Jijini Dodoma tarehe 10 Agosti, 2025.

Chapisha Maoni

0 Maoni