Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro imetoa wito kwa watanzania
kutembelea vivutio vinavyosimamiwa na mamlaka hiyo ili kujifunza masuala
mbalimbali kuhusu wanyama na malikale.
Afisa Uhifadhi Mkuu Masoko NCAA, Michael Makombe ameeleza hayo kwa kuwa wananchi wanaotembelea maonesho
ya nanenane yanayofanyika katika viwanja
vya Nzughuni mjini Dodoma na kuongeza kuwa;
“Tunatumia maonesho haya kuwaelimisha watembeleaji kuhusu upekee wa
Ngorongoro kama sehemu yenye utajiri wa vivutio vya utalii, kuwaelezea gharama
za kuingia hifadhini, fursa za uwekezaji, uhifadhi shirikishi na historia ya
binadamu na makabila yanayoishi kiasili Tanzania ,”alisema Bw.Makombe.
Afisa Uhifadhi Mkuu, urithi wa Utamaduni na Jiolojia PCO Ramadhan Hatibu
ameeleza kuwa wananchi wanaotembelea maonesho hayo pia wanapata elimu ya kujua
vivutio vya urithi wa utamaduni, chimbuko la binadamu wenye umri wa zaidi ya
miaka 3.6 iliyopita, kupata habari za eneo la Olduvai lenye masalia ya viumbe
hai walioshi zaidi ya miaka Mil 2 iliyopita na kujua Jamii za makabila ya
wamaasai, Wadatoga, Wahadzabe na wairaq ambapo wageni wanaotembelea Ngorongoro
wanaweza kuona Jamii za makabila hayo zinavyoishi maisha yao ya asili na
kulinda utamaduni wao.
PCO Hatibu ameeleza kuwa Ngorongoro ni eneo muhimu ambalo ni urithi wa
dunia ikiwa sehemu pekee katika nchi za Ukanda wa Afrika kuwa hadhi 3 kwa
pamoja ambazo World Herritage Site, Biosphere Reserve na Urithi wa kijiolojia
(UNESCO Global Geopark) na kutumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi kutembelea
hifadhi ya Ngorongoro kwa ajili ya kujifunza na kuona utajiri wa Dunia uliopo
katika hifadhi hiyo.
Na. Mwandishi wa NCAA - Dodoma
0 Maoni