Mbunge wa Jimbo la Kisesa mkoani Simiyu kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Luhaga Mpina ameonekana kwenye vikao na viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo na
kuibua uvumi wa uwezekano wa kujiunga na chama hicho.
Inasemekana chama hicho kimeridhia mwanasiasa huyo kujiunga nacho ili
kupeperusha bendera yake katika nafasi ya kuwania Urais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.
Mpina ambaye alienguliwa na CCM katika mchakato wa kuwania kuteuliwa
kugombea ubunge anasemekana kuamua kubadilisha jukwaa la kufanyia siasa na sasa
huenda akawa mgombea wa Urais kwa tiketi ya ACT Wazalendo.
Chama cha ACT Wazalendo kinatarajiwa kufanya mkutano wake mkuu tarehe 6
Agosti 2025 kwa ajili ya kumpitisha mwanachama atakayepeperusha bendera ya
chama hicho katika nafasi ya Urais mwaka huu.

0 Maoni