Mtiania urais kwa chama cha ACT Wazalendo achukua fomu ZEC

 

Mtiania wa kiti cha urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud amekabidhiwa fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania kiti hicho na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi katika ofisi za tume hiyo zilizopo Maisara, Unguja Zanzibar leo Jumapili Agosti 31, 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa fomu hiyo, Othman amesema lengo la kuwania kiti hicho ni kutaka kuwatumikia Wazanzibari ambao wamemwandaa kwa muda mrefu, hivyo umefika wakati wa kurejesha imani kwao.

Amesema ACT Wazalendo wanatarajia kufanya kampeni zitakazokuwa za amani ni wajibu wa kila Mzanzibari kuhakikisha usalama na amani vinakuwapo wakati wote wa mchakato wa uchaguzi huku akisisitiza msimamo wa chama chake wa kutokubaliana na kura ya mapema akidai sheria hiyo haifai.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Mhe. Jaji George J. Kazi leo tarehe 31 Agosti, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mtiania wa Kiti cha Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka Chama cha Kijamii (CCK), Mhe. Isha Salim Hamad , Hafla hiyo imefanyika katika Afisi za Tume zilizopo Maisara Wilaya ya Mjini Unguja.


Chapisha Maoni

0 Maoni