Mke wa rais wa zamani wa Korea Kusini
aliyefungwa, Yoon Suk Yeol, amekamatwa kwa mashtaka kadhaa, ikiwa ni pamoja na
udanganyifu wa hisa pamoja na rushwa.
Aliyekuwa mama wa taifa, Kim Keon Hee,
alikana mashtaka yote wakati wa kikao cha saa nne cha Mahakama kilichofanyika
mjini Seoul siku ya Jumanne.
Hata hivyo, Mahakama ilitoa hati ya
kumuweka kizuizini, ikitaja uwezekano wa yeye kuharibu ushahidi.
Korea Kusini ina historia ya marais wa
zamani kufunguliwa mashtaka na kufungwa jela. Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza
kwa rais wa zamani pamoja na mkewe wote wawili kufungwa.
Yoon alikamatwa mwezi Januari ili
kufikishwa mahakamani kwa jaribio la kutekeleza sheria ya kijeshi
lililoshindikana mwaka jana, ambalo liliingiza nchi katika machafuko na
hatimaye kusababisha kuondolewa kwake madarakani.
Rais wa zamani wa Korea Kusini
aliyefungwa, Yoon Suk Yeol akiwa na mkewe Kim Keon Hee wakati akiwa madarakani
kama Rais wa Korea Kusini.
0 Maoni