Miili mitano imefukuliwa kwenye makaburi mapya ambayo
yanahisiwa kuwa na uhusiano na kundi la kidini lililowaaminisha waumini wake kufa
kwa njaa ili waingie peponi la nchini Kenya.
Katika mojawapo ya matukio mabaya zaidi ya vifo vya halaiki
vinavyohusishwa na madhehebu ya kidini, zaidi ya miili 400 iligunduliwa mwaka
2023 katika Msitu wa Shakahola, ulioko maeneo ya ndani kutoka mji wa pwani wa
Malindi.
Inaaminika kuwa watu hao walikuwa wafuasi wa Mhubiri
aliyejipatiwa wadhifa mwenyewe, Paul Mackenzie, ambaye anadaiwa kuwahamasisha wafuasi
wake wajinyime chakula hadi kufa.
Ugunduzi huu wa hivi karibuni unaonekana kuthibitisha hofu
iliyotolewa na serikali mapema mwaka huu kwamba kundi hilo bado linaweza kuwa
linaendelea na shughuli zake kwa siri.
Mwezi Aprili, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kipchumba Murkomen, alisema kulikuwa na madai kuwa Mackenzie alikuwa akiwasiliana na wafuasi wake kutoka gerezani akitumia simu ya mkononi.
0 Maoni