Mafuriko ya ghafla yaliyosababishwa na
mvua kubwa yameua zaidi ya watu 400 katika maeneo mbalimbali ya Pakistan,
Kashmir inayosimamiwa na India, na Nepal, kwa mujibu wa mamlaka, huku watu
wengi wakiwa bado hawajapatikana.
Kaskazini magharibi mwa Pakistan, watu
wasiopungua 321 wamefariki ndani ya kipindi cha saa 48, mamlaka za mitaa
ziliripoti Jumamosi, huku vijiji zaidi ya kumi katika eneo la Buner, mkoa wa
Khyber Pakhtunkhwa, vikiwa vimeharibiwa vibaya na mafuriko ya ghafla.
Barabara zilizosombwa na maporomoko ya
ardhi zimewazuia wahudumu wa dharura kufika katika maeneo yaliyoathirika huko
Buner, ambako inahofiwa kuwa watu wengine kadhaa wamefukiwa chini ya vifusi,
kwa mujibu wa Bilal Faizi, Msemaji wa Shirika la Uokoaji la Rescue 122.
"Zaidi ya miili 120 tayari imeopolewa
kutoka eneo hili pekee. Hadi siku chache zilizopita, hapa palikuwa na jamii hai
na yenye shughuli. Sasa, hakuna kilichobaki zaidi ya mawe makubwa na mabaki ya
uharibifu," Faizi aliwaambia waandishi wa habari.
0 Maoni