Mgombea Udiwani wa Kata ya Vingunguti Kupitia Chama Cha
Mapinduzi (CCM), Omary Kumbilamoto ambae
anatetea nafasi hiyo leo amechukua fomu ya kugombea kiti hicho katika ofisi ya Kata ya
Vingunguti.
Kumbilamoto ambaye alisindikizwa na
umati mkubwa wa watu aliweza kuchukua fomu hiyo Majira ya saa 9:40 asubuhi chini
ya uangalizi wa katibu Kata Wa CCM Mama Agatha.
Mara baada ya kuchukua fomu hiyo
Kumbilamoto alijinasibu Kwa kusema kuwa anaimani kubwa ya kushinda uchaguzi huo
kutokana utekelezaji mkubwa wa ilani uliofanyika katikati kata ya Vingunguti.
"Katika miaka mitano tuliyopewa
dhamana na wana Vingunguti CCM tumefanya makubwa mengi kuanzia miundombinu ya
barabara, masoko,huduma za Afya na kuwafikia wananchi mmoja mmoja katika
mahitaji yao," amesema Kumbilamoto.
Ametaja Kuwa katika miaka yake mitano
ya Udiwani amewezesha kupatikana kwa Ambulance katika zahanati ya Vingunguti,
Soko la kisasa la nyama Choma, Machinjio na Mabucha ya Kisasa pamoja na
barabara za zege mitaani.
Amesema kuwa CCM inakaribisha wagombea
wa vyama vya upinzani kuweka wagombea wao waje washindane kwa
hoja sio matusi.
0 Maoni