Kamishna wa Uhifadhi
Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) Abdul-razaq Badru amesema mamlaka hiyo
Kwasasa itajikita katika kuendeleza ubunifu ili mapango ya Amboni yaliyoko
mkoani Tanga yaweze kuvutia wageni wengi kutoka ndani na nje ya Nchi.
Katika mazungumzo yake na
watendaji wa kituo hicho Kamishna Badru amesema eneo hilo ni hazina na
kinachohitajika ni kulitumia kama fursa ya kiuchumi kupitia shughuli za utalii.
“Tushirikiane kwa umoja
wetu na tubuni miradi ambayo italifanya eneo la Amboni liwe na mvuto kwa wageni
wetu kutoka ndani na nje ya nchi,”alisema Kamishna Badru.
Mapango ya Amboni
yamebeba hazina yenye historia mbalimbali ikiwemo harakati za kudai uhuru wa
Tanzania bara,urithi na utamaduni wa makabila na watu wa Tanga pamoja na
mafunzo ya jiografia ambapo ni adimu kupatikana katika nchi
nyingine duniani.
Na. Hamis Dambaya -
Amboni Tanga
0 Maoni