Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Bw. Charles
Kichere ametembelea kijiji cha Msomera kwa lengo la kuangalia ujenzi wa
miundombinu mbalimbali inayojengwa na
Serikali katika kijiji hicho.
Katika ziara hiyo CAG Kichere amekagua nyumba 1,500 ambazo
tayari zimekamilika kwa ajili ya Wananchi wanaotokea Ngorongoro kuhamia kijiji
cha msomera kwa hiari sambamba na kukagua miradi ya barabara, maji, shule na
huduma za afya, umeme na maeneo ya mifugo kama minada na malisho.
Mkuu wa wilaya ya Handeni mhe. Salum Nyamwese ameipongeza
serikali kutokana na jitihada kubwa za uwekezaji katika kijiji hicho ambacho
kimekuwa cha mfano Tanzania.
Katika ziara hiyo Bw. Kichere alifuatana na Kamishna wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro bwana Abdul-Razaq Badru pamoja na watendaji wengine wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali, Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.
0 Maoni