WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa, leo tarehe 22 Julai 2025, ameendelea na ziara yake rasmi nchini
Belarus kwa kutembelea maeneo muhimu ya uzalishaji na ushirikiano wa kimkakati.
Akiwa katika mji wa
Minsk, Mheshimiwa Majaliwa alitembelea kiwanda cha Belmedpreparaty, ambacho ni
maarufu kwa utengenezaji wa dawa za binadamu.
Aidha, Waziri Mkuu pia
alitembelea kiwanda cha Minsk Tractor Plant, ambacho kinajihusisha na
utengenezaji wa matrekta na mitambo ya kisasa ya zana za kilimo. Ujumbe wa
Tanzania ulijionea teknolojia ya hali ya juu inayotumika katika uzalishaji wa
vifaa hivyo.
Wakati wa ziara hiyo,
pamoja na viongozi wengine, Waziri Mkuu aliambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Cosato Chumi.
Mheshimiwa Majaliwa pia
aliweka shada la maua katika mnara wa mashujaa wa Jamhuri ya Beralus.
Kwa ujumla, ziara hiyo ni
sehemu ya jitihada za Serikali ya Tanzania kuimarisha mahusiano ya kimataifa
kwa manufaa ya wananchi, hasa katika sekta muhimu za maendeleo kama afya na
kilimo.

0 Maoni