Waziri wa Maliasili na
Utalii mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana (mb)
amewapongeza watendaji wa wizara hiyo kwa kutimiza malengo ya ilani ya Chama
cha Mapinduzi (CCM) kwa kufikisha idadi ya watalii milioni tano kama
ilivyoainishwa kwenye ilanı ya chama hicho.
Dkt.Chana ametoa pongezi
hizo katika uzinduzi wa siku maalum ya Ngorongoro (Ngorongoro Day) ikiwa ni
sehemu ya maadhimisho ya maonesho ya 49 ya biashara ya kimataifa Sabasaba.
“Niwapongeze sana
watendaji wenzangu wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na wadau wa sekta ya
utalii kwani ilanı ya CCM ilitutaka tufikishe watalii milioni tano na sasa
tunatembea kifua mbele kwani idadi hiyo imetimia.”
Waziri Chana pia
ameipongeza Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) kwa kuvuka lengo la
makusanyo kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa kukusanya shilingi bilioni 269.9
kutoka lengo la shilingi bilioni 230.
Akitoa maelezo ya siku
hiyo ya Ngorongoro Meneja wa huduma za utalii na Masoko Bi Mariam Kobelo
amesema lengo kubwa ni kuunga mkono juhudi za mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan za kutangaza utalii na kupata
wageni wengi zaidi.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania Ephraim Mafuru amesema bodi hiyo kwa
kushirikiana na taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na utalii
zitaendelea kushirikiana ili kuhakikisha kuwa idadi ya watalii na mapato ya
serikali kupitia sekta hiyo yanaongezeka.
Na. Mwandishi wa NCAA - Dar es Salaam
0 Maoni