Serikali ya Korea
Kusini kupitia shirika la KOICA imeandaa Mkutano wa Kimataifa kubadilishana
uzoefu kwenye kuboresha mifumo ya usimamizi wa huduma za afya kwa kutumia
teknolojia ya kisasa.
Mkutano huu
umehusisha watalaam kutoka Tanzania na Korea ikiwa ni sehemu ya ushirikiano wa
Mradi wa Kupanua matumizi ya Mfumo wa GOTHOMIS unaotelekelezwa Mkoani Dodoma.
Akizungumza kwa niaba
ya ujumbe wa Tanzania, Mkurugenzi Msaidizi - (Huduma za Lishe) Bw. Lutifrid
Nnally, amesema ushiriki wa Tanzania unalenga kujifunza uzoefu wa Korea kwenye
matumizi ya mifumo ya kidijitali katika huduma za afya.
Tanzania inatarajia
kutumia uzoefu huo kufanya maboresho ya GOTHOMIS, kuimarisha ushirikiano wa
kimataifa, na kuongeza ufanisi wa utoaji huduma kwa kutumia teknolojia kama
telemedicine, akili bandia (AI) na mifumo ya taarifa za kiafya.
Ushiriki huu ni hatua
muhimu katika mageuzi ya sekta ya afya, hasa kwa maeneo ya vijijini, ili
kuhakikisha huduma bora, za haraka na kwa gharama nafuu
zinawafikia wananchi wote.
Na. Angela Msimbira - Seoul, Korea
0 Maoni