Shirika la Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA) linashiriki Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya
Sabasaba kwa ajili ya kutangaza vivutio vya utalii, fursa za uwekezaji na
kuelimisha umma umuhimu wa kuhifadhi Maliasili kwa faida ya Tanzania na dunia
kwa ujumla. Katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi uhifadhi wa mimea ni
jambo ambalo TANAPA pia italipa kipaumbele ili kuwa na mazingira rafiki na
salama kwa binadamu na wanyamapori.
Karibu we mwananchi
katika Banda la TANAPA upate elimu ya Uhifadhi, ujue umuhimu wa utalii na ofa
mbalimbali za kutembelea Hifadhi za Taifa katika kipindi hiki cha Msimu wa
Sabasaba.
Aidha, shirika hilo
litaendelea kutumia jukwaa hilo kuonesha jitihada mbalimbali zilizofikiwa
katika kudumisha mahusiano mema na jamii zinazozunguka hifadhi hizo
zilizohifadhi tunu mujarabu za Taifa.
Maonesho hayo
yaliyoanza rasmi June 28, 2025 yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai 04, 2025
huku kauli mbiu ikiwa ni “SabaSaba
Fahari ya Tanzania.”



0 Maoni