Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Jeshi
la Umoja wa Visiwa vya Comoro alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Bergamo Moroni leo tarehe 06 Julai 2025.
Rais Dkt. Samia yupo
katika Umoja wa Visiwa vya Comoro kwa Ziara ya kikazi ya siku moja ambapo pia
amealikwa kama Mgeni Rasmina na Rais wa nchi hiyo Mhe. Azali Assoumani
kuhudhuria Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa nchi hiyo
zitakazofanyika kwenye Uwanja wa Malouzini Omnisport mjini Moroni.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono wananchi alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bergamo Moroni leo tarehe 06 Julai 2025.
0 Maoni