Mamlaka ya Hifadhi ya
eneo la Ngorongoro (NCAA) inatumia fursa ya mkutano wa pili wa mabaraza huru ya
Habari Afrika unaofanyika jijini Arusha kunadi vivutio vya utalii vilivyopo
Ngorongoro ili kuendelea kuwavutia wageni wengi zaidi.
Mkutano huo unaofanyika
Jijini Arusha kuanzia tarehe 14- 17 Julai 2025 unawakutanisha wadau mbalimbali
wa Sekta ya Habari kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika ambapo washiriki zaidi
ya 200 wanahudhuria mkutano huo.
Afisa Utalii Mkuu NCAA
Peter Makutian ameeleza kuwa ushiriki wa NCAA katika mkutano huo unalenga
kuwafikia wajumbe wa mkutano huo na kuwaelezea vivutio vya utalii vilivyopo
Ngorongoro ambayo ni kivutio Bora cha Utalii Afrika kwa mwaka 2023 na mwaka 2025.
"Kama mnavyojua
Ngorongoro ni kivutio Bora cha utalii Afrika hivyo wageni wanahamasika na kuwa
na shauku ya kujua vivutio vilivyopo,
fursa za uwekezaji na shughuli za utalii, kwa siku zote za mkutano huu
tutahakikisha tunawafikia na kuendelea kutangaza eneo letu" alisema Makutian.
Kauli mbiu ya mkutano huo
ni; "Kuendeleza kanuni za vyombo
vya habari na mawasiliano kwa ubora wa uandishi wa habari barani Afrika."
Na. Kassim Nyaki - NCAA
0 Maoni