Ayoub Alexander
mtumishi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ni mmoja wa
washiriki wa Msafara wa Twende Butiama ulioanza leo tarehe 3 hadi 13 Julai,
2025.
Lengo la Msafara huo
wa kusafiri kutumia Baiskeli ni kumuenzi
kwa Vitendo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika harakati
mbalimbali ikiwemo kupigania uhuru.
Mtumishi huyo kupitia
msafara wa waendesha Baiskeli unaonzia Dar es Salaam na kupita mikoa ya Tanga,
Kilimanjaro, Arusha, Manyara hadi Butiama Mkoani Mara wenye Km 1541
anaipeperusha Bendera ya eneo la hifadhi ya Ngorongoro ambalo ni kivutio Bora
cha Utalii Afrika 2025.
Ngorongoro
Conservation Area: Africa's Number One Attraction 2025.



0 Maoni