Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa ameupongeza uongozi wa Shule ya Sekondari ya Kibaha kwa kuendelea kuwa na matokeo ya ufaulu mzuri huku akiwataka kutoshuka.
Mhe. Mchengerwa
ametoa kauli hiyo jana wakati alipotembelea shule hiyo na kukagua miundombinu ya madarasa, mabweni,maabara na
baadaye kushuhudia wanafunzi waliokuwa wakijiunga na kuzungumza na walimu wa
shule hiyo.
Waziri Mchengerwa
amesema ameridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na walimu hao kwani katika
kipindi chote shule imekuwa miongoni mwa shule zenye matokeo mazuri nchini.
Amesema kutokana na
ongezeko la wanafunzi wa kidatu cha tano kwa mwaka huu, walimu wanatakiwa
kuweka mikakati madhubuti ili kuhakikisha wanabaki katika kiwango kilekile cha
ufaulu.
"Natambua safari
hii tumeongeza wanafunzi wa kidato cha tano hakikisheni mnakuja na mikakati
ambayo itamaintain kiwango kilekile," amesisitiza Mhe. Mchengerwa.
Kwa mujibu wa Afisa
Elimu wa Mkoa wa Pwani Jimmy Daudi Nkwamu ufaulu wa kidatu cha sita mwaka huu
ni asilimia 93.7 ambapo wanafunzi 136 kati ya wanafunzi 140 wqmepaata daraja la
kwanza.
Kwa upande wa matokeo
ya kidatu cha nne kwa mwaka 2024 amesema
asilimia 52 ya wanafunzi wote walipata daraja la kwanza huku kukiwa hakuna
daraja la tatu, nne na sifuri.
Aidha, Mhe.
Mchengerwa amemuelekeza Afisa Elimu wa Mkoa wa Pwani kuhakikisha anafanya ziara
katika wilaya zote za Mkoa huo na
kubaini changamoto zote ili kuzipatia ufumbuzi.
"Ninakutaka
kutoka ofisini na kwenda kwenye Wilaya zote kuona kama kuna changamoto na kutafuta ufumbuzi mara moja," amefafanua
Waziri Mchengerwa.
Na. John Mapepele -
Kibaha
0 Maoni