Chama cha Mapinduzi (CCM)
kimeingiza kiasi cha shilingi 2,737,500,000 kutokana na ada za fomu za kuwania
ubunge.
Kiasi hicho cha fedha
kimetokana na ada za watia nia 5,475 waliochukua fomu za kuwania ubunge katika
majimbo mbalimbali. Ada ya fomu moja ni shilingi 500,000.
Kiasi hiki
kinadhihirisha mshikamano na hamasa kubwa ya wanachama wa CCM kushiriki
mchakato wa uchaguzi wa ndani wa chama, ambao ni hatua muhimu kuelekea uchaguzi
mkuu ujao.
CCM imeendelea
kusisitiza umuhimu wa mchakato wa uchaguzi ndani ya chama kufanyika kwa uwazi
na haki ili kuhakikisha wagombea bora na wenye sifa wanapata nafasi ya kuwania
nafasi mbalimbali za uongozi.
0 Maoni