WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa leo Juni 20, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro (MUM), kwenye viwanja vya chuo hicho mkoani Morogoro.
Maadhimisho hayo ni
jukwaa la kutathmini historia, changamoto, mafanikio yaliyopatikana na mchango
wa chuo hicho katika maendeleo ya Taifa.
Pia, Maadhimisho hayo
yamelenga kuakisi changamoto na maendeleo ya chuo hicho katika kipindi cha miaka 20 ya kutoa maarifa, nidhamu, na malezi
bora ya vijana wa Kitanzania
0 Maoni