Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe; Balozi. Dkt Pindi H. Chana (Mb) anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika tukio la kihistoria la utoaji wa tuzo za Utalii duniani kanda ya afrika ambazo zitafanyika leo tarehe 28 Juni, 2025 katika Hoteli ya hadhi ya nyota tano ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam.
Hafla hiyo
inayotarajiwa kuanza saa 12:30 za jioni na kuisha 05:00 za usiku itahidhuriwa
pia na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe;
Dunstan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt Hassan
Abbas, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe; Albert chalamilla, viongozi wa
vyombo vya Ulinzi nchini pamoja na viongozi
wa taasisi mbalimbali za Serikali na sekta binafsi.
Katika tukio
hilo, zaidi ya washiriki 500 kutoka
mataifa mbalimbali watahudhuria ambapo tukio hilo pia litakuwa mubashara (Live) kupitia vyombo vya
habari mbalimbali ili kuwezesha
watanzania na watu wengine
ulimwenguni kufuatilia tukio hilo
adhimu na la kihistoria hapa nchini.
Vyombo vya habari
ambavyo vitarusha tukio hilo mubashara ni pamoja na Tanzania Safari Channel,
Azam TV, ITV, ZBC, Tbc Digital, Utalii TV, Clouds TV, Tanzania Unforgettable,
Tanzania Parks na mitandao ya kijamii mbalimbali.

0 Maoni