Wananchi wa kata ya Buseresere wilayani Chato mkoani Geita wameeleza kunufaika na ujenzi wa barabara ya Maweni yenye urefu wa km 1.5 kwa kiwango cha changarawe.
Akiongea katika
mahojiano maalum Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Chato, Mhandisi Edgar Kidasi
ameeleza kuwa kazi zilizofanyika katika eneo hilo ni pamoja na kuchonga
barabara, kunyanyua tuta, kumwaga kifusi na kujenga mitaro ili maji yapate
uelekeo sahihi kipindi cha mvua.
"Eneo hili
lilikuwa korofi hasa kipindi cha mvua na ukizingatia kwamba barabara hii
inawasaidia wananchi kufika Hospitali, shuleni na eneo la soko ambapo hapo
awali palikuwa hapapitiki lakini sasa wananchi wanapita bila shida yoyote,"
amesema Mhandisi Kidasi.
Naye, Bw. Deus Musiba
mkazi wa Buseresere ameeleza kuwa kwa kipindi kirefu barabara hiyo ilikuwa
kikwazo kwa wananchi hasa kuzifikia huduma za kijamii ambapo wanafunzi walikuwa
hawawezi kwenda shule kipindi cha masika lakini kwa sasa njia inapitika katika
kipindi chote cha mwaka.
Kwaupande wake, Bi.
Yustina Robert mkazi wa Buseresere ameipongeza Serikali kwa hatua hiyo ya
kuondoa vikwazo katika barabara na kuwezesha wananchi kusafiri kwa urahisi.
"Kwasasa
wanafunzi wanaenda shule kwa urahisi hata sisi tunafaya kazi zetu bila kikwazo
cha barabara tofauti na hapo awali," amesema Bi. Yustina.
0 Maoni