Ofisi ya Rais –
TAMISEMI imewakutanisha Makatibu Tawala Wasaidizi Sehemu za Mipango Uratibu,
Uchumi na Uzalishaji, Wakuu wa Idara za mipango na uratibu na waweka hazina wa
Halmashauri katika mafunzo maalum ya pamoja kuhusu uendeshaji na usimamizi wa
miradi ya maendeleo.
Akifungua mafunzo
hayo jana June 3, 2025 Jijini Dodoma, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI Bw.
Adolf Ndunguru amesema mafunzo hayo ni sehemu ya kuwaandaa vyema maafisa viungo
hao muhimu katika utendaji kazi wa Serikali katika Mamlaka za Serikali za Mikoa
na Tawala za Mitaa ili kuwa tayari katika utekelezaji wa vipaumbele vya bajeti
ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Katibu Mkuu Ndunguru
ameyataja maeneo yatakayogusiwa katika mafunzo hayo kuwa ni ugharamiaji wa
miradi kwa njia mbadala - (AlternativeFinancing), mwongozo wa makampuni mahsusi
ya kuanzisha na kusimamia miradi ya vitega uchumi vya Halmashauri (SPV –
Special Purpose vehicle), Malipo kwa nijia ya internet banking na ukusanyaji wa
Mapato na Usuluhishi wa Kibenki (Revenue collection and Reconciliation).
Awali Mkurugenzi wa
Sera na Mipango Ofisi ya Rais TAMISEMI Bw. John Cheyo, amesisitiza umuhimu wa
mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kujifunza namna bora ya utekelezaji wa masuala
kadha mapya ambayo ni sehemu ya ubunifu katika bajeti ya mwaka 2025/2026.
0 Maoni