Serikali imefunga shughuli za Kanisa la Glory of Christ Church maarufa kama Kanisa la Ufufuo na Uzima linaloongozwa na Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima kwa kutoa mahubiri yenye mwelekeo wa kisiasa na nia ya kuichonganisha serikali na wananchi.

Taarifa aliyoitoa leo Msajili wa Jumuiya za Kiraia Emmanuel Kihampa na nakala kwenda kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura, imesema vitendo hivyo ni kinyume cha Sheria ya Jumuiya Sura ya 337 na vinaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.