Katibu Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akiwasili katika Uwanja
wa Ndege wa Songea, mkoani Ruvuma na kupokelewa na viongozi wa Chama na
Serikali mkoani humo, wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Ahmed Abbas
Ahmed na Katibu wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mohamed Ali Khalfan, leo Jumatatu tarehe
2 Juni 2025.
Balozi Nchimbi
amewasili mjini Songea, kwa ajili ya kushiriki mazishi ya mwanasiasa mkongwe na
mmoja wa wapigania uhuru wa Tanganyika, na waasisi wa Chama cha TANU na CCM,
Alhaj Mzee Mustafa Mohamed Songambele, aliyefariki usiku wa kuamkia Juni 1,
2025 jijini Dar es Salaam na kutarajiwa kuzikwa leo mjini Songea.
0 Maoni