Serikali imetoa
shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika
maeneo mbalimbali ya kimkakati kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa
wabunge kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa
leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge
katika kipindi cha maswali na majibu kwa
niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Akijibu swali la
nyongeza la Mhe. Dorothy Kilave mbunge wa jimbo la Temeke aliyetaka kujua hatua
zilizochukuliwa na serikali katika kujenga kituo cha afya kata ya Sandali jimbo
la Temeke Mhe. Dkt. Dugange amesema licha ya serikali kujenga vituo vya afya
katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Temeke lakini itaendelea kutenga fedha ili
kuhakikisha kata zote za kimkakati zinakuwa na vituo vya afya.
“Serikali inaendelea
kuboresha huduma za afya kote nchini na niwahakikishie waheshimiwa wabunge kuwa
hii ni dhamira ya dhati ya serikali kuhakikisha inasogeza huduma za afya karibu
na wananchi na itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga vituo vya afya
katika kata zote za kimkakati,” alisema Mhe. Dkt. Dugange.
Serikali yatoa Tsh.
bilioni 30 kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya kata za kimkakati.
Serikali imetoa
shilingi bilioni 30 kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa vituo vya afya katika
maeneo mbalimbali kwenye majimbo 120 yaliyoainishwa na waheshimiwa wabunge
kupitia bunge la Jamahuri ya Muungano wa Tanzania.
Kauli hiyo imetolewa
leo (June 02, 2025) bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mhe. Dkt. Festo Dugange wakati akijibu maswali ya waheshimiwa wabunge
katika kipindi cha maswali na majibu kwa
niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI Mhe. Mohamed
Mchengerwa.

0 Maoni