Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu
Mteule wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Mhandisi Machibya Shiwa, mapema leo
Juni 26, 2025 kabla Mheshimiwa Rais hajasafiri na Treni ya SGR kwenda Dodoma.
Hii ni mara ya kwanza
kwa Mkurugenzi Mkuu mteule wa TRC Mhandisi Machibya, kukutana na Mhe. Rais
Samia akiwa katika wadhifa wake mpya toka ateuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa TRC Juni 23, 2025.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan ameelekea Jijini Dodoma
ambapo Pamoja na mambo mengine kesho Juni 27, 2025 anarajiwa kuhutubia na
kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
0 Maoni