Waziri Chana atembelea Ofisi ya Wizara ya Kilimo Zanzibar

 

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) Juni 25, 2025 alitembelea Ofisi ya Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo iliyopo Zanzibar na alipokelewa na mwenyeji wake, Katibu Mkuu wa wa Wizara hiyo Ali Khamis Juma.

Waziri Chana aliambatana na Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) ikiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mej. Jen (Mstaafu) Hamis Semfuko.

Mazungumzo kati ya Waziri Chana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo, Ali Khamis Juma yalijikita katika maeneo mbalimbali yakiwemo kupanga mikakati ya kukuza utalii nchini kati ya Wizara hizo mbili pamoja na kuangalia fursa za uwekezaji wa Bustani ya Wanyamapori Zanzibar iliyopo katika Hifadhi ya Jambiani Muyuni iliyopo Mkoa wa Kusini.





Chapisha Maoni

0 Maoni