Eneo la Hiafadhi ya
Ngorongoro limetangazwa na kushinda tuzo ya kuwa kivutio bora cha utalii Barani
Afrika kwa mwaka 2025.
Ngororngoro imeibuka
kidedea katika tuzo za World Travel Awards (WTA) zilizofanyika jana usiku tarehe 28 Juni, 2025 katika hoteli ya Johari
Rotana Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Pindi
Chana.
Ngorongoro imevishinda
vivutio vingine vya utalii ambavyo ni
Harbeespoort Aerial Cableway, V & AWaterfront, Table Mountain na
Kisiwa cha Robben za Afrika Kusini, Pyramids of Giza ya Misri, ziwa Malawi na
Mlima Kilimanjaro.
#TanzaniaShines
#Ngorongoroshines
0 Maoni