Watu kadhaa
wanahofiwa kupoteza maisha baada ya kutokea ajali iliyohusisha basi la kampuni
ya Channel One lililokuwa likisafiri kutokea Moshi kuelekea Tanga kugongana uso
kwa uso na basi dogo aina ya Coaster lililokuwa likitoka wilayani Same.
Mkuu wa Wilaya ya
Same, Mhe. Kasilda Mgeni amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Sabasaba Kata
ya Same, wilayani Same, mkoani Kilimanjaro, na magari yote mawili yalilipuka
moto na kuteketea.
0 Maoni