Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) inashiriki katika Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma
yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, jijini Dodoma, kuanzia tarehe
16 hadi 23 Juni 2025.
Tunawakaribisha
wananchi wote ndani ya Mkoa wa Dodoma, taasisi za Serikali na binafsi na
makundi mbalimbali kututembelea banda la NCAA lililopp kwenye banda la Wizara
ya Maliasili na Utalii waweze kupata elimu kuhusu uhifadhi,
shughuli za utalii na maendeleo ya jamii hususan ushirikishwaji wa jamii
kwenye sekta ya uhifadhi na utalii.
“Wiki ya Utumishi wa Umma, Huduma imesogezwa karibu yako, Karibu tukuhudumie.”
0 Maoni