Hospitali ya Taifa
Muhimbili Upanga na Mloganzila imesogea karibu na wananchi kwa kushiriki katika
Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja
vya Sabasaba kuanzia tarehe 28 Juni hadi 13 Julai mwaka huu.
Ushiriki huu unalenga
kutoa huduma za afya kwa wananchi kwa urahisi pamoja na kutoa elimu kuhusu
namna bora ya kujikinga na magonjwa mbalimbali katika banda namba 16, lililopo
Mtaa wa Maonesho Avenue.
Huduma zinazotolewa
ni pamoja na uchunguzi wa magonjwa ya macho na uoni hafifu pamoja na huduma za
miwani, uchunguzi na matibabu ya magonjwa ya masikio, pua na koo, pamoja na
uchunguzi wa afya ya uzazi na magonjwa ya kina mama,huduma za radiolojia,
matibabu ya magonjwa ya dharura, vipimo vya maabara pamoja na huduma ya
ushonaji kwa wanaohitaji huduma hizo.
Hospitali ya Taifa
Muhimbili inaendelea kutumia maonesho ya Sabasaba kama jukwaa la kusogeza huduma
za afya karibu na wananchi na kuhamasisha umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya
mara kwa mara ili kujikinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika mapema.
0 Maoni