MDAU wa Maendeleo
Mkoa wa Iringa, Wakili Sosten Mbendule amempongeza Chifu Adam Sapi Mkwawa II
kwa kuwaleta pamoja katika kuadhimisha tamasha la utamaduni la Wahehe.
Wakili Mbedule
amesema tamasha hilo la Wahehe lililoanza Juni 16 na kufikia kilele chake leo
Juni 19, 2025 katika kijiji cha Kalenga
mkoani Iriga linasaidia kudumisha
utamaduni wa kabila la Wahehe na kukemea mmomonyoko wa maadili hususani katika
suala la mavazi.
Amesema, kuanzishwa
kwa tamasha hilo mila, desturi za tamaduni za wahehe zitahimarika kwani
zilishaanza kupotea ikiwa ni pamoja na kuhamasisha elimu ya kulinda utu wa mtu.
“Tamasha hili ni
lizuri limeleta chachu ya matumizi ya
biadhaa za uzalishaji wa kilimo, utalii na huduma mbalimbali za usafirishaji
fedha na bima,” amesema.
Pia limesaidia
kuwaleta pamoja vijana, wanawake na wazee
katika kulinda na kuendeleza urithi
wa tamaduni za wahehe nchini.
Katika maadhimisho
hayo yamefanyika matambiko ya kimila katika maeneo ya kihistoria ya mto Mkwawa
na wahehe kwa ujumla, kutatembelea maeneo ya kihistoria lengo ni kukuza utamaduni wao.
0 Maoni