WAZIRI MKUU, Kassim
Majaliwa leo Juni 23, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye
kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja
vya Chinangali Park Jijini Dodoma.
Katika hafla hiyo,
Mheshimiwa Majaliwa atazindua mifumo miwili ambayo ni Mfumo wa kielektroni
unaowezesha mifumo ya Serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa, ujulikanao
kama *Government Enterprises Service Bus (GovESB)* na Mfumo wa pili ni wa
e-Wekeza unaomuwezesha Mtumishi wa Umma kuwekeza katika Mfuko wa Faida (Faida
Fund).
Siku ya Utumishi wa
Umma husherehekewa kila Juni 23 kila mwaka na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika
kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya nchi zao
na Bara la Afrika kwa ujumla.
Kaulimbiu ya
maadhimisho hayo ni “Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijiti ili Kuongeza
Upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza Uwajibikaji.”



0 Maoni