Maandalizi ya Mac D
Bonanza 2025 & Fun Run (Mbio za kujifurahisha) yamekamilika kwa asilimia
kubwa huku washiriki wa mbio za kujifurahisha wakivuka lengo la wakimbiaji
lililowekwa jambo linaonyesha kuwapo na mwamko kubwa wa watu kushiriki tamasha
hilo litakalofanyika Juni 7, 2025.
Akiongea leo Jijini
Dar es Salaam kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi
wa Eb Twenty Five, Mratibu wa Mac D Bonanza Denzel Rweyunga amesema wamefurahishwa
na namna jamii ilivyohamasika katika kushiriki Bonanza hilo kwa mwaka huu.
“Sisi waandaaji tulijiwekea
lengo la kupata washiriki wa mbio za kujifurahisha 700 tu, lakini kutokana na
mwamko mkubwa wa jamii na hamasa iliyokuwapo mitaani hadi kufikia leo tuna
idadi ya washiriki zaidi ya 1,800,” alisema Denzel.
Amesema kwamba kwa
sasa zoezi la kutoa fulana bure na namba za washiriki waliojisajili kwa ajili ya
kukimbia mbio za Kilomita 10 na Kilomita 5 nalo linaenda vizuri ambapo
washiriki wengi wameshachukua fulana zao katika vituo mbalimbali tayari kwa
maandalizi mbio.
Ameeleza kuwa mgeni
rasmi wa Mac D Bonanza 2025, ambalo litafanyika katika viwanja vya Chuo Cha
Taifa cha Ulinzi (NDC) Kunduchi, likishirikisha mbio za kujifurahisha, burudani
na baadae jioni mchezo wa soka kati ya
Mac D FC na IPP Media, atakuwa Mhe. Hamis Mwinjuma, Naibu Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Kwa upande wake Mjumbe
wa Kamati ya Maandalizi Calvin Obeld amesema amesema kwamba mbio zitaanza 12:00
asubuhi kwa mbio za Kilomita 10 na kufuatiwa na mbio za Kilomita 5, ambapo zitaanzia katika viwanja vya Chuo cha Taifa
cha Ulinzi (NDC) kilichopo Kunduchi na kuhitimishwa katika viwanja hivyo hivyo.
Mac D Bonanza 2025
inadhaminiwa na Bodi ya Utalii Tanzania ( TTB ), Isumba Trans Limited ( ITL ),
Kilimanjaro Water, Namis Corporate Limited, JC Hall, Zakys Bay, Pwani Inland
Clearance Deport Ltd PICD) na EB Twenty Five na ITV & Radio One.
0 Maoni