Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi
ametembelea Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Uswisi, ikiwa ni ziara yake ya
kikazi nchini humo, lengo ni kushiriki Jukwaa la Nane la Dunia la Kupunguza
Madhara ya Maafa linalofanyika kuanzia tarehe 2 hadi 6 Juni, 2025 Jijini Geneva
Nchini Uswisi.
Dkt. Yonazi ameongoza
ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki Mkutano huo huku
akiambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Brigedia Jenerali
Hosea Ndagala, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu,
Ofisi hiyo Stella Mwaiswaga, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini, Ofisi ya
Waziri Mkuu Charles Msangi pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Menejimenti
ya Maafa sehemu ya Utafiti, Ofisi hiyo Vonyvaco Luvanda.
Aidha, amepokelewa na
kufanya mazungumzo na Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Ofisi
za Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Kimataifa Geneva Uswisi Dkt.
Abdallah Possi na kumweleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika Jukwaa hilo
unatija na manufaa makubwa kwa Taifa.
Amefafanua kuwa
Jukwaa hilo linalenga kutathmini, kujadili maendeleo ya utekelezaji wake na
kuimarisha masuala ya usimamizi wa maafa kimataifa kupitia makubaliano ya
hiyari ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa ambayo yameridhiwa.
Sambamba na hilo,
Dkt. Yonazi ameupongeza ubalozi huo na kuahidi kuendeleza ushirikiano masuala
mbalimbali ili kuona fursa zilizopo Uswisi na kuzichangamkia fursa za
kibiashara sambamba za zinazoendana na mabadiliko ya Kiteknolojia.
Akitoa maelezo kuhusu
utekelezaji wa shughuli za ubalozi, Dkt. Possi amesema amepongeza ushiriki wa
Tanzania katika Jukwaa hilo la Nane na kusisitiza kuwa Tanzania ina kila sababu
ya kuendelea kushiriki katika mikutano hiyo ili kuwa na mwendelezo mzuri
utakaowezesha nchi kupata na kutumia fursa mbalimbali zinazotokana na Majukwaa
hayo.
0 Maoni