Kamishna wa Uhifadhi
TANAPA, Musa Nassoro Kuji jana tarehe 21 Juni, 2025 alifanya ziara ya kikazi na
kufanya kikao na Maafisa na Askari wa Hifadhi ya Taifa Gombe na Milima ya
Mahale zilizopo Kigoma.
Kikao ambacho
kilijikita katika kuboresha utendaji kazi wa kila siku.
Katika kikao hicho
Kamishna Kuji alisisitiza bidii zaidi katika kufanya kazi, nidhamu na uadilifu
na kubainisha kuwa mafanikio yanayopatikana katika Shirika la Hifadhi za Taifa
Tanzania (TANAPA) ni matokeo ya nidhamu, bidii, na uadilifu miongoni mwa
Maafisa na Askari wa Uhifadhi katika kutekeleza majukumu ya Shirika.
“Nitoe pongezi zangu
kwa mafanikio ambayo Shirika limeyafikia kwa mwaka huu utakaoisha tarehe 30
Juni, 2025 tumevuka malengo. Mpaka sasa Shirika limevuka malengo ya makusanyo
ya mapato yaliyokusudiwa kukusanywa kwa mwaka wa fedha husika. Haya yote ni
matokeo ya uadilifu, nidhamu na kujituma kwa kila mmoja wetu katika kutekeleza
majukumu yetu,” alisema Kamishna Kuji.
Akiwasilisha taarifa
ya hifadhi, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Yustin Njamasi ambaye ni Mkuu wa
Hifadhi ya Taifa Gombe alimpongeza Kamishna wa Uhifadhi kwa kutenga muda wake
na kwenda kuwatembelea kusikiliza na kujadili kwa pamoja mikakati ya namna bora
ya kukuza uhifadhi na kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za utalii.
Pia, Kamishna Njamasi
ameipongeza Bodi ya Wadhamini TANAPA pamoja na Menejimeti ya Shirika kwa namna
ambavyo imekuwa ikiwasaidia katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Kamishna
Njamasi alimkabidhi Kamishna wa Uhifadhi tuzo ambayo ilitolewa kwa TANAPA kwa
kuthamini mchango wa TANAPA katika kusaidia watu wenye ulemavu wa ngozi nchini
iliyotolewa na Chama cha Watu Wenye Ulemavu wa Ngozi Tanzania na kukabidhiwa na
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).
Kwa upande wake,
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Halid Mngofi ambaye ni Mkuu wa Hifadhi ya Taifa
Milima ya Mahale kwa mwaka fedha ujao imejidhatiti vilivyo katika kuhifadhi na
kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo pamoja mapato yatokanayo na shughuli za utalii.
Hifadhi ya Taifa
Gombe na Milima ya Milima ya Mahale zilizopo Mkoani Kigoma zina umaarufu mkubwa
unaotokana na uwepo wa idadi kubwa ya wanyama aina ya Sokwe Mtu.
0 Maoni