Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana kwa furaha na Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.
Ridhiwani Jakaya Kikwete huku Baba yake Rais Mtaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya
Kikwete akifurahi nao.
Tukio hili adimu limetokea
kwenye sherehe za ufunguzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye
urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 katika eneo
la Chuo cha ufundi Kalwande, Kigongo wilayani Misungwi mkoani Mwanzatarehe 19 Juni, 2025.
0 Maoni