Dkt. Possi afungua mafunzo ya watumishi ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali

 

Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati akifungua mafunzo kwa watumishi hao yaliyofanyika Jijini Arusha.

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akitoa neno la utangulizi wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Jijini Arusha.

Dakitari Bingwa wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Garvin Kweka akitoa mada kuhusu namna ya kukabiliana na msongo wa mawazo wakati wa mafunzo kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali yaliyofanyika Jijini Arusha.

Mratibu wa Kusimamia Magonjwa yanayoambukiza wa Ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Aisha Zukheri akitoa mada kuhusu Magonjwa yanayoambukiza kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Arusha.

Mkufunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania, Dkt. Hosea Njovango akitoa mada kuhusu Maadili ya Utumishi wa Umma kwa watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali Jijini Arusha.

Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakimsikiliza Wakili Mkuu wa Serikali, Dkt. Ally Possi (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano mkuu kwa watumishi wa Ofisi hiyo  Jijini Arusha.

Chapisha Maoni

0 Maoni