Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Maliasili na Utalii anayesimamia Maliasili CP. Benedict Wakulyamba
amefunga mafunzo ya Mafisa na Askari wa Jeshi la Uhifadhi NCAA yaliyofanyika
katika kituo cha Mafunzo ya jeshi la Uhifadhi Mbulumbulu Wilaya ya Karatu
Mkoani Arusha.
Akifunga mafunzo hayo
yenye wahitimu 25 wanaojumuisha Naibu Kamishna mmoja (01), Makamishna Wasaidizi
waandamizi wanne (04), Maafisa Uhifadhi wakuu kumi (10), Afisa Uhifadhi waandamizi watano (05), afisa
uhifadhi daraja kwanza wawili (02), askari uhifadhi mkuu 01 na askari uhifadhi
daraja la pili (02) CP. Kamishna Wakulyamba amewasisitiza wahitimu hao
kuzingatia uwajibikaji katika Utumishi kwa kufuata taratibu, nidhamu ya kijeshi
na kutumia vyeo walivyonavyo kama nyenzo ya utawala katika mfumo wa Kijeshi.
“Natumia fursa hii
kuwapongeza wahitimu wote 25 kwa kuhitimu mafunzo haya muhimu ya mabadiliko ya
utendaji, hakikisheni mnazingatia , maadili,
uadilifu, ujasiri, uzalendo, nidhamu, uadilifu kuzingatia amri na
nidhamu za kijeshi na kuongeza ubunifu katika usimamizi wa rasilimali za misitu
na wanyamapori na kuhakikisha kuwa mnaendelea kupata mafunzo ya mara kwa mara
na kutumika ipasavyo katika maeneo yenu” alisisitiza Wakulyamba.
Akitoa taarifa kuhusu
mafunzo hayo Mkuu wa Mafunzo hayo Kanali Fikiri Machibya ameeleza kuwa mafunzo
kwa maafisa na askari hao yalijikita katika Uongozi wa kijeshi, Kwata, matumizi
ya Silaha ndogo (SMG & PistoL, Itifaki na maadili, Ulinzi wa viongozi,
General order (GO) na ulengaji shabaha.
Akizungumza kwa niaba
ya Kamishna wa Uhifadhi Naibu kamishna wa Uhifadhi NCAA, Joas Makwati ameeleza
kuwa mafunzo yaliyotolewa kwa watumishi hao ni fursa kujifunza kwa nadharia na
vitendo juu ya mabadiliko ya mfumo wa kiraia kwenda katika mfumo wa kijeshi.
Ameongeza kuwa
mafunzo hayo yamewabadilisha viongozi, maafisa na maaskari wa uhifadhi katika
kuwajibikaji kwenye majukumu ya kila siku kwa kuzingatia misingi ya kijeshi,
nidhamu na utiifu na kubainisha kuwa uongozi wa NCAA utaendelea kuendesha
mafunzo ya mara kwa mara kwa maafisa na askari wa jeshi la uhifadhi.
Mratibu wa Jeshi la
Uhifadhi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii
Kamishna Msaidizi Mwandamizi Fidelis Kapalata ameeleza kuwa Wizara hiyo
inaendelea kuhakikisha kuwa watumishi wote wa taasisi za Uhifadhi zilizoko
chini ya Wizara hiyo zinaendelea kupata mafunzo ya mara kwa mara ili
kujiimarisha katika udhibiti wa vitendo vya ujangili na kuwa imara mda wote
katika kuzilinda rasilimali za wanyamapori na misitu.
Na. Kassim Nyaki- Karatu Arusha
0 Maoni