Chama cha Mapinduzi
(CCM), kimetuma salamu za pole kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na
familia zilizopoteza watu 28 na wengine saba kujeruhiwa katika ajali iliyotokea
Mlima Iwambi jijini Mbeya.
Salamu hizo za pole
zimetolewa katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili Juni 8,2025 na Katibu wa
Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, Amos Makalla, ambayo imesema CCM inaungana
na Watanzania wote kuwaombea marehemu wapumzike kwa amani.
0 Maoni