Bodi ya Wakurugenzi
ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imekutana leo Juni 23,
2025 Jijini Dar es Salaam Kwa ajili ya kuanza kikao chake cha Kawaida cha 31
cha Bodi hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Meja Jenerali (Mstaafu) Hamis R. Semfuko.
Ikiwa ni siku ya
kwanza, wajumbe wa kamati ya Ulinzi wa Rasilimali ya Wanyamapori na Uendeshaji
na Usimamizi wa Rasilimali watu inayoongozwa na Prof. Jafari Kideghesho na
Kamati za Sera, Mipango na Fedha inayoongozwa na Dr. Simon Mduma wamekutana na kujadili masuala mbalimbali yanayoihusu
utendaji kazi wa TAWA.
0 Maoni