Katibu Mkuu wa Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameongoza mamia ya
waombolezaji, katika utoaji wa heshima za mwisho na hatimae mazishi ya Mzee
Silvin Ibengwe Emmanuel Mongella, mwenza wa mmoja wa viongozi waandamizi
wastaafu nchini, Bi. Getrude Mongella, leo Jumamosi tarehe 7 Juni 2025, katika
Kijiji cha Kabusungu, Ilemela, mkoani Mwanza.
Shughuli hiyo ya
mazishi ya Mzee Mongella, ambaye pia ni baba mzazi wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM
(Bara), Ndugu John Mongella, ilitanguliwa na ibada ya misa takatifu
iliyofanyika nyumbani kwa marehemu, ikiongozwa na Askofu Mkuu Renatus Leonard
Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, huku mahubiri yakitolewa na Padri
George Nzungu.
Mbali ya Balozi Dkt.
Nchimbi, viongozi wengine waliojumuika pamoja na waombolezaji katika mazishi
hayo ni pamoja na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia
ni Rais wa Jumuiya ya Mabunge Duniani (IPU), Dkt. Tulia Ackson Mwansasu,
mawaziri, viongozi waandamizi wa Chama na Serikali, wabunge na viongozi wa
kiroho kutoka madhehebu ya dini mbalimbali nchini.
0 Maoni