Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb) amenadi vivutio vya utalii vya
nchini Tanzania huku akikaribisha wawekezaji kutoka nchini Japan kuwekeza Tanzania.
Waziri Chana amesema
hayo leo Mei 26, 2025 katika Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii
lililofanyika katika Hoteli ya The Westin jijini Osaka nchini Japan.
"Tanzania ni
moja ya nchi ambayo ina utulivu wa kisiasa chini ya uongozi mahiri wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hivyo nawakaribisha
kuwekeza katika maeneo mbalimbali ya utalii," amesisitiza Mhe. Chana.
Aidha, amewahasisha
wadau wa utalii nchini Japan kudumisha uhusiano wa Biashara ya utalii kati ya
Wakala wa Utalii wa nchini humo na Tanzania na kuitembelea Tanzania ili kukuza
na kuendeleza Sekta ya Utalii.
Kongamano hilo
lilifunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa aliyeongoza ujumbe wa
Tanzania kushiriki katika Maonesho ya Expo 2025 Kansai
Osaka nchini Japan.
0 Maoni