Rais wa Marekani,
Donald Trump, amemuita Vladimir Putin "mwendawazimu kabisa" kufuatia
mashambulizi makubwa ya anga ya Urusi dhidi ya Ukraine yaliyofanywa mwishoni
mwa wiki.
"Anaua watu
wengi bila sababu, na sizungumzii tu wanajeshi. Makombora na droni yanapigwa
kwenye miji ya Ukraine bila sababu yoyote," Trump aliandika kwenye mtandoa
wake wa jamii siku ya Jumapili.
Ingawa hasira zake
zilielekezwa hasa kwa rais wa Urusi, Trump pia alikuwa na maneno makali kwa
Zelensky, akisema kuwa "hafanyi lolote la msaada kwa nchi yake kwa
kuzungumza jinsi anavyofanya."
Usiku wa Jumamosi,
Urusi ilirusha droni na makombora 367 dhidi ya Ukraine, shambulizi kubwa zaidi
la anga dhidi ya Ukraine tangu kuanza kwa uvamizi kamili mwaka 2022. Watu
wasiopungua 12 waliuawa.
0 Maoni