Serikali kupitia Programu Jumuishi ya
Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto (PJT-MMMAM) imefanikiwa
kuanzisha vituo 206 vya kijamii vya kulelea watoto wadogo mchana na kusajili
vituo binafsi 4,178 nchi nzima tangu mwaka 2021.
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa, Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza, Mhe. Said Mtanda, amesema vituo hivyo vinahudumia jumla ya watoto
11,675 huku vya binafsi vikihudumia watoto 6,154.
Aidha, jumla ya walezi 445 wamepatiwa
mafunzo ya malezi na makuzi ili kuhakikisha utoaji bora wa huduma katika vituo
hivyo. Mtanda alisisitiza kuwa uwekezaji katika malezi ya awali ni msingi wa
kukuza rasilimali watu yenye tija kwa familia na taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Bw. Sebastian Kitiku, amesema mkutano
wa tathmini wa siku mbili unawaleta pamoja Maafisa Lishe kutoka Tanzania Bara
na Zanzibar pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili mafanikio na changamoto
za utekelezaji wa programu hiyo.
Naye, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za
Ustawi wa Jamii, Bi. Subisya Kabuje, amesisitiza kuwa washiriki wa mkutano huo
wamejipanga kuibua njia bora za kuimarisha utekelezaji wa PJT-MMMAM.
Na. OR-TAMISEMI
0 Maoni