Maambukizi ya kisonono yaongezeka Uingereza, kutoa chanjo

 

Uingereza itakuwa nchi ya kwanza duniani kuanza kuwapatia watu chanjo dhidi ya maambukizi ya kwa njia ya ngono ya ugonjwa wa kisonono.

Chanjo hii haitapatikana kwa kila mtu. Lengo kuu litakuwa kwa wanaume mashoga na wale wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia zote mbili (bisexual), hasa waliokuwa na historia ya kuwa na wapenzi wengi au waliowahi kuambukizwa magonjwa ya zinaa.

Chanjo hiyo ina ufanisi wa kati ya asilimia 30 hadi 40, lakini Shirika la Taifa la Huduma za Afya la England NHS linatumaini kwamba itasaidia kupunguza ongezeko kubwa la maambukizi.

Kulikuwa na zaidi ya kesi 85,000 mwaka 2023 – idadi ya juu zaidi tangu kuanza kwa takwimu mwaka 1918.

Kisonono huwa hakioneshi dalili kila mara, lakini baadhi ya dalili zake ni maumivu, kutokwa na usaha usio wa kawaida, uvimbe sehemu za siri, na utasa.

Chapisha Maoni

0 Maoni