Nguli wa fasihi ya
Kingereza Ngũgĩ wa Thiong'o, raia wa Kenya amefariki dunia akiwa na umri wa
miaka 87.
Ngũgĩ alitazamiwa
kushinda Tuzo ya Nobel ya Fasihi mara nyingi, na kuwaacha mashabiki wakiwa na
masikitiko kila mara tuzo hiyo alipoikosa.
Atakumbukwa si tu
kama mwandishi aliyestahili Nobel, bali pia kama mtetezi shupavu wa fasihi
iliyoandikwa kwa lugha za asili za Kiafrika.
Ngũgĩ alizaliwa kwa
jina James Thiong’o Ngũgĩ mwaka 1938, wakati Kenya ilikuwa chini ya utawala wa
kikoloni wa Waingereza.
Alikulia katika mji
wa Limuru miongoni mwa familia kubwa ya wafanyakazi wa kilimo wa kipato cha
chini.
0 Maoni